Mwakinyo Bado ameshikiliwa

 

 Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga linaendelea na uchunguzi wa tukio la bondia Hassan Mwakinyo (29) anyetuhumiwa kwa kumjeruhi na kumshambulia mvuvi Mussa Ally (21) mkazi wa Sahare Jijini Tanga 

Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi amesema baada ya tukio hilo wameanza uchunguzi huku wakiendelea kumshikilia Mwakinyo. 

Kamanda Mchunguzi amesema kwamba tukio hilo lilitokea Machi 4 mwaka huu nyumbani kwa Hassan Mwakinyo ambapo baada ya uchunguzi wa shauri  hilo kukamilika watamfikisha mahakamani kwa taratibu za kisheria. 

"Mara baada ya uchunguzi wa shauri hili kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria," amesema Kamanda huyo wa Polisi mkoani Tanga

Kwa mujibu wa Kamanda Mchunguzi amesema Mwakinyo baada ya kuhojiwa alieleza kwamba, "Huyo mtu alimchukulia kama mwizi lakini kumchukulia mtu kama hivyo haimpi mtu mamlaka ya kumchukulia sheria mkononi ndio maana Jeshi la Polisi linamshikilia kuendelea kuchunguza kujua kiini cha kumshambulia mtu huyo,".

Aidha ameongeza kuwa, "Lakini kumekuwepo kwa tuhuma mbalimbali zinazomtuhumu Mwakinyo kufanya vitendo kama hivyo miaka ya nyuma Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi na kama kuna mtu ana taarifa hizo za nyuma azilete nitazifanyia kazi," amesema RPC.

Habari Zilizotrendi:

Zungu Spika Mpya wa Bunge la Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali mpya

MWIGULU NCHEMBA NDIYE WAZIRI MKUU MTEULE