Nicole apandishwa Kizimbani
Msanii wa Bongo Movie, Joyce Mbaga maarufu "Nicole Berry' leo Machi 10 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka mbalimbali yakiwemo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia akaunti yake ya Whatsap.
Nicole amefikishwa katika mahakama hiyo ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam liripoti kumshikilia kwa tuhuma hizo.
Machi 3 mwaka 2025 baadhi ya watu walijitokeza hadharani wakidai kutapeliwa na Nicole na kisha kuzima simu zake.
.jpeg)