BILIONI 18 KUWASHA UMEME VITONGOJI RUVUMA



Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeimarisha usimamizi wa miradi ya kusambaza umeme vitongojini mkoani Ruvuma kwa lengo la kuhakikisha vitongoji vyote nchini vinapata nishati hiyo ifikapo mwaka 2030.

Wakati wa ziara ya ukaguzi mkoani humo Februari 01, 2026, Meneja wa Usimamizi wa Miradi ya REA, Mha. Deogratius Nagu, amebainisha kuwa wakala huo unakagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kujionea maendeleo yake halisi.
Mhandisi Nagu amemuelekeza mkandarasi, kampuni ya MF Electrical Engineering Ltd, kuongeza kasi ya ujenzi wa Mradi wa Ujazilizi Fungu 2C unaohusisha wilaya za Songea, Mbinga, na Nyasa.
Hadi sasa, vitongoji 88 kati ya 148 vimeshawashiwa umeme, huku mkandarasi akitakiwa kukamilisha haraka usambazaji katika vitongoji 60 vilivyosalia ili wananchi waanze kunufaika na huduma hiyo.
Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 18.294 na unatarajiwa kunufaisha wateja wa awali wapatao 6,781 mkoani Ruvuma.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesisitiza kujipanga kikamilifu kukamilisha miradi hiyo kwa wakati, huku mkandarasi akiahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na REA ili kufanikisha azma ya Serikali ya kufikisha umeme vijijini.

Habari Zilizotrendi:

MWIGULU NCHEMBA NDIYE WAZIRI MKUU MTEULE

Rwanda yajaribu programu inayotegemea akili bandia (AI) kuboresha huduma za afya kwa wakazi

Uganda: Washington yaghadhabishwa na kauli za mkuu wa jeshi ambaye ni mtoto wa rais