Ujumbe wa Rais Samia kwa Rais wa Zambia



 Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama siku ya jana March 24, 2025 amewasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Haikainde Hichielema katika Ikulu ya Rais iliyopo Jijini Lusaka Zambia.

Rais Hichielema amemshukuru Rais Samia kwa ujumbe huo maalum na kubainisha ya kuwa Zambia na Tanzania ni nchi zenye historia na ushirikiano wa kindugu muda mrefu na usio na mipaka.
Waziri Mhagama akiwa ameambatana na ujumbe wake akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Generali Mathew Edward Mkingule amemshukuru Rais Hichielema kwa mapokezi mazuri na ushirikiano imara ulipo baina ya Tanzania na Zambia

Habari Zilizotrendi:

Zungu Spika Mpya wa Bunge la Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali mpya

MWIGULU NCHEMBA NDIYE WAZIRI MKUU MTEULE