Maafisa na Askari JWTZ Wavishwa nishani
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Jacob Mkunda, kwa niaba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan, amewavisha nishani mbalimbali maafisa na askari wa JWTZ jijini Mbeya leo, Machi 26, 2025. Akizungumza baada ya kuvisha nishani hizo, Jenerali Mkunda amewapongeza maafisa na askari waliotunukiwa kwa jinsi Rais Samia Suluhu Hassan alivyotambua mchango wao katika kulitumikia taifa kwenye nyanja ya ulinzi. Aidha, amewataka maafisa na askari kuendelea kuviishi viapo vyao na kuhakikisha mipaka yote ya nchi inabaki salama wakati wote. Nishani walizotunukiwa askari hao ni Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne, Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ, na Nishani ya Jumuiya ya SADC