Madagascar: Kimbunga Fytia kimesababisha kifo cha mtu mmoja na zaidi ya watu 8,000 wameathiriwa

 Madagascar ambayo imekumbwa na kimbunga Fytia kwa siku mbili, tangu Jumamosi Januari 31 hadi Jumapili Februari 1, sasa inajaribu kutathmini uharibifu uliosababishwa na kimbunga hicho. Ingawa uharibifu unaweza kuonekana mdogo, hasa huko Antananarivo, wakazi wa vitongoji kadhaa katika mji mkuu bado wanaishi katika mafuriko.

Kimbunga Fytia kilivuka Madagascar kutoka magharibi hadi mashariki mwishoi mwa wiki hii iliyopita. Kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka Ofisi ya Kitaifa ya Usimamizi wa Majanga na Maafa (BNGRC), kimunga Fytia kimesababisha mmoja kifo cha mtu mmoja, mwengine mmoja hajulikani alipo, na karibu watu 8,400 wameathiriwa. Baada ya kutua alfajiri Jumamosi, Januari 31, karibu na Majunga kaskazini-magharibi mwa kisiwa hicho, kikiambatana na upepo mkali unaofikia hadi kilomita 210 kwa saa, kimbunga hicho kilirudi baharini, kikiwa kimepunguza kasi na kuwa kimbunga cha wastani cha kitropiki, kutoka pwani ya mashariki asubuhi ya Jumapili, Februari 1.

Wakati huo huo, kmunga hiki kilipiga katika mji mkuu, Antananarivo, ambapo mvua kubwa ilinyesha usiku kucha. Katika baadhi ya vitongoji, kuliripotiwa mafuriko, na kulazimisha wakazi kupanda mikokoteni kwa gharama ya ariary 300  (sawa na senti 50 za euro) ili waweze kuvuka mitaa iliyojaa maji kabisa.

Wilaya ya 4, imejaa maji kila kona- wakati mwingine maji hufikia hadi magotini. watu wengi wanateseka na hali hiyo, kama Sehène, bibi anayeishi na wajukuu zake wawili. Alilazimika kuhama nyumba yake katikati ya usiku, na kugundua asubuhi, siku iliyofuata kwamba moja ya kuta zake ilianguka, anasema hana "mahali pa kwenda" alipoona uharibifu huo, huku akisema ana wasiwasi mkubwa kutokana na hali hiyo.

Katikati ya hali ya mlipuko wa Mpox, umakini mkubwa wa kiafya umewekwa. Katka mji wa Antananarivo, uharibifu huu unaweza kuonekana kuwa mdogo. Lakini kwa familia ambazo nyumba zao zimeharibiwa, uharibifu huu unaonyesha ugumu mwingine katika maisha ya kila siku ambayo tayari ni hatari. Kwa kujibu, BNGRC tayari imeahidi "kukabiliana" na hali hiyo, ikibainisha kwamba pampu za kuondoa maji yaliyotuama zitapatikana kwa wale wanaozihitaji, ingawa mifereji ya jiji iliyozeeka hujaa maji haraka.

Kutokana na hali hii, mamlaka pia inawasihi wakazi wa mji mkuu kuwa macho zaidi kuhusu tahadhari za kiafya, kwani Antananarivo pia inakabiliwa na mlipuko wa Mpox ambao unaweza kuzidisha hali hiyo katika siku zijazo.

Habari Zilizotrendi:

MWIGULU NCHEMBA NDIYE WAZIRI MKUU MTEULE

Rwanda yajaribu programu inayotegemea akili bandia (AI) kuboresha huduma za afya kwa wakazi

Uganda: Washington yaghadhabishwa na kauli za mkuu wa jeshi ambaye ni mtoto wa rais