Uganda: Washington yaghadhabishwa na kauli za mkuu wa jeshi ambaye ni mtoto wa rais

 Marekani lazima itathmini upya ushirikiano wake wa usalama na Uganda, Jim Rish kutoka chama cha Republican, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Baraza la Seneti, ametangaza kwenye mtandao wa kijamii  wa X.

Msururu wa jumbe zilizochapishwa kwenye jukwaa hilo la X na Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambapo alishutumu ubalozi wa Marekani mjini Kampala kwa kumsaidia kiongozi wa upinzani Bobi Wine kutoroka nyumbani kwake wakati wa uvamizi wa jeshi, muda mfupi baada ya uchaguzi wa urais Januari 15.

Kufuatia kuchapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X kwa machapisho kadhaa na mkuu wa jeshi la Uganda—ambaye pia ni mtoto wa rais Yoweri Museveni—mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Baraza la Seneti la Marekani ameghadhabishwa. Jenerali Kainerugaba amevuka mstari: Marekani sasa lazima itathmini upya ushirikiano wake wa usalama na Uganda, Jim Rish aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Sababu? Msururu wa jumbe kutoka kwa Jenerali Muhoozi Kainerugaba ulishutumu ubalozi wa Marekani mjini Kampala kwa kumsaidia kiongozi wa upinzani Bobi Wine kutoroka wakati wa uvamizi wa jeshi nyumbani kwake jioni ya yalipokuwa yakitangazwa matokeo ya uchaguzi wa urais wa Januari 15. Pia alitangaza kusitishwa kwa ushirikiano wote na ubalozi wa Marekani nchini Uganda.

Ingawa Kainerugaba, anayejulikana kwa aina hii ya uchochezi, amefuta ujumbe wake kwenye ukurasa wake wa X na kuomba radhi - "Nilizungumza na balozi wa Marekani na kila kitu kiko sawa. Tutaendelea na ushirikiano wetu wa kijeshi," alisema Jenerali Muhoozi Kainerugaba - msamaha huu hauonekani kuwashawishi wengi huko Washington. "Mtoto wa rais—ambaye pia ndiye mrithi wake—hawezi kufuta jumbe kwenye ukurasa wake wa X na kuomba msamaha wa uongo," Seneta Jim Risch alisema, akiongeza, "Marekani haitavumilia kiwango hiki cha kutokuwa na utulivu na kutowajibika."

Habari Zilizotrendi:

MWIGULU NCHEMBA NDIYE WAZIRI MKUU MTEULE

Rwanda yajaribu programu inayotegemea akili bandia (AI) kuboresha huduma za afya kwa wakazi