MWIGULU NCHEMBA NDIYE WAZIRI MKUU MTEULE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu amempendekeza aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kinachosubiriwa kwa sasa baada ya jina kuwasilishwa kwa Spika wa Bunge ni mchakato wa kuthibitishwa kwa jina hilo na bunge