Mazungumzo ya Marekani na Iran yaanza

Wawakilishi wa Marekani leo wanatarajiwa kufanya mazungumzo na wenzao wa Iran huko Muscat, Oman kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. Upande wa Marekani, mjumbe maalum Steve Witkoff na Jared Kushner, mkwe wa Rais Donald Trump, watashiriki. Ajenda halisi ya mkutano huo bado haijulikani. Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema Iran inapania kuyawekea mipaka mazungumzo hayo yajikite katika mpango wa nyuklia wa Iran na kulegezwa kwa vikwazo. Marekani ingependa kuongeza mada zaidi kwenye ajenda, ikiwa ni pamoja na mpango wa makombora wa Iran na msaada kwa washirika wake, ikiwa ni pamoja na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza, wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon na waasi wa Houthi nchini Yemen.


Habari Zilizotrendi:

MWIGULU NCHEMBA NDIYE WAZIRI MKUU MTEULE

Rwanda yajaribu programu inayotegemea akili bandia (AI) kuboresha huduma za afya kwa wakazi

Uganda: Washington yaghadhabishwa na kauli za mkuu wa jeshi ambaye ni mtoto wa rais