Rwanda yajaribu programu inayotegemea akili bandia (AI) kuboresha huduma za afya kwa wakazi
Mradi huoI ambao unaitwa Horizon 1000, uliotengenezwa na Wakfu wa Gates na kampuni ya Marekani ya OpenAI kwa ushirikiano na mamlaka ya Rwanda, unalenga kushughulikia uhaba mkubwa wa wataalamu wa afya nchini. Ikiwa imejaribiwa kwa miaka miwili katika kliniki zipatazo hamsini za Rwanda, programu hiyo inaweza kutumwa katika vituo 1,000 vya afya kote barani Afrika ikiwa matokeo yatakuwa ya uhakika.
Je, akili bandia (AI) inaweza kuboresha upatikanaji na ubora wa huduma za afya? Nchini Rwanda, Wakfu wa Gates kwa sasa unazindua programu ya majaribio ya programu mpya iliyoundwa ili kuwasaidia wataalamu wa afya katika kufanya maamuzi yao. Nchi hii inakabiliwa na uhaba mkubwa wa wafanyakazi wa afya na miundombinu, hasa katika maeneo ya vijijini: Rwanda ina daktari mmoja tu kwa kila wagonjwa 1,000, huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likipendekeza mara nne ya idadi hiyo.
Kwa kutumia teknolojia inayotegemea akili bandia (AI), programu hiyo inatumwa katika kliniki 50 kwa kipindi cha miaka miwili. Mradi huo, unaofanywa kwa ushirikiano na mamlaka za Rwanda, unaoitwa Horizon 1000—ambapo Wakfu wa Gates na kampuni ya Marekani ya OpenAI wanawekeza dola milioni 50, "unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma na kuimarisha—si kuchukua nafasi ya uamuzi wa kimatibabu," anaelezea Andrew Muhire, afisa mkuu katika Wizara ya Afya ya Rwanda.
Ingawa lengo la programu hii ni kuwasaidia wataalamu wa afya kuboresha maamuzi yao na kuokoa muda, kipindi cha majaribio kitakachopitia lazima kishughulikie suala kubwa: programu hii ilundwa na kuendelezwa kwa Kiingereza, lugha isiyozungumzwa sana nchini Rwanda, ambapo 75% ya raia huwasiliana kwa Kinyarwanda.
Bado haijabainika kama matokeo yatakuwa ya uhakika. Ikiwa ndivyo, programu hiyo inaweza kupelekwa katika vituo vya afya 1,000 kote barani Afrika.