Vipimo 5,600 vyakutwa na Dosari


 Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) umefanya uhakiki wa vipimo milioni 3.6 katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye mita za maji, vituo vya kuuzia mafuta na mitungi ya gesi, katika kipindi cha miaka minne ambapo katika uhakiki huo vipimo 100,005 vilikutwa na mapungufu na kurekebishwa na vipimo vingine 5,600 vilikutwa na dosari.

Mtendaji Mkuu wa WMA, Albani Kiula amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wakala huo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita.
Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Wakala wa Vipimo litakalorahisisha, kuboresha na kusogeza huduma karibu na wananchi.

Habari Zilizotrendi:

Maafisa na Askari JWTZ Wavishwa nishani

Watumishi wa umma Uganda washurutishwa kufanya mazoezi kila wiki

Waziri Mkuu afanya ukaguzi wa viwanja