Timu za uokoaji kwa kushirikiana na wakaazi wa eneo la milima ya Jebel Marra jimbo la Darfur zinaendelea na juhudi za kuopoa miili, ingawa wanakumbwa na changamoto kubwa kutokana na ukosefu wa vifaa na ukubwa wa janga hilo. Kulingana na takwimu rasmi idadi ya watu waliopoteza maisha katika mkasa huo inakadiriwa kuwa kati ya watu 300 na 1,000. Baraza la mpito la uongozi wa kijeshi chini ya usimamizi wa Jenerali Abdel Fattah al-Burhan limeahidi kuhamisha raslimali zote zilizopo ili kusaidia waathiriwa, wakati serikali pinzani ikitangaza iko tayari kuanza juhudi za kutoa misaada.
Wizara ya Afya imetoa taarifa yake ambapo imeonyesha ongezeko la watu wenye maambukizi ya ugonjwa wa Uviko-19 nchini katika kipindi cha mwezi Februari hadi Aprili mwaka huu. Takwimu hizo zimetolewa leo Jumanne Mei 20, 2025, na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Grace Magembe kupitia taarifa yake kwa umma, ambapo amesema kumekuwepo ongezeko la tetesi zinazohusiana na magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa katika jamii nchini. “Hali ya kuongezeka na kupungua kwa ugonjwa huu imekuwepo kila mwaka tangu kutangazwa kwa ugonjwa huu mwaka 2020. Kwa kipindi hiki ongezeko hili linaonekana zaidi katika Mkoa wa Dar es Salaam,” amesema Dk. Magembe. Dk. Magembe amesema kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya mfumo njia ya hewa, wizara imebaini kuna ongezeko la wagonjwa wenye Uviko-19 kutoka wawili kati ya watu 139 waliopimwa Februari sawa na asilimia 1.4 hadi wagonjwa 31 kati ya watu 185 waliopimwa Aprili mwaka huu, sawa na asilimia 16.8. “Tangu Februari hadi Aprili 2025, ufuatiliaji wa viru...
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalumu George Mkuchika ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini mkoani Mtwara ametangaza rasmi kutogombea ubunge katika uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu. Waziri Mkuchika ametangaza uamuzi huo kwenye kikao cha kamati kuu ya jimbo kilichokuwa na lengo la kuzungumzia mafanikio ya jimbo hilo.