Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefungia kwa muda dimba la Benjamin Mkapa lililopo Dar es Salaam kutokana na eneo la kuchezea (pitch) kuendelea kupungua ubora wake. CAF imeelekeza maboresho ya uwanja huo yafayike haraka kufikia viwango vinavyotakiwa ili kuepuka Uwanja huo kufungiwa kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kati ya Simba SC dhidi ya Al Masry, imepangwa kuchezwa kwenye uwanja huo Aprili 9, 2024, hivyo basi CAF imelielekeza Shirikisho hilo kutuma jina la uwanja mbadala utakaotumiwa na vijana hao wa Msimbazi kufikia Machi 14, 2025. CAF imepanga kufanya ukaguzi katika uwanja huo wa Benjamin Mkapa, Machi 20, 2025 ili kuona maboresho yaliyofanyika kabla ya kufanya maamuzi ya matumizi yake.