Posts

DARAJA LA MAGUFULI KUANZA KAZI MWEZI APRIL

Image
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt. Charles Msonde amesema daraja la J.P Magufuli (Kigongo Busisi) lenye urefu wa KM 3 litaanza kutumika rasmi Aprili 30 mwaka huu. Hata hivyo, amesema ifikapo Aprili 10, 2025 magari yataanza kupita upande mmoja kwenye daraja hilo ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 97 huku ujenzi wake ukigharimu zaidi Shilingi ya bilioni 610. Daraja hilo limejengwa kwa lengo la kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara - Sengerema Geita KM90 ambayo ni sehemu ya barabara iliyopo kwenye Ushoroba wa Ziwa Victoria inayoanzia Sirari mpakani mwa Tanzania na Kenya hadi Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda. Kwa sasa sehemu ya barabara hiyo eneo la Kigongo Busisi inaunganishwa kwa kutumia vivuko vikubwa vitatu vya MV Mwanza, MV Misungwi na MV Sengerema. Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 3 na upana wa meta 28.45 lina njia mbili za magari zenye upana wa mita 7 kila upande.

Mkuchika atangaza kutogombea Ubunge

Image
  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalumu George Mkuchika ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini mkoani Mtwara ametangaza rasmi kutogombea ubunge katika uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu. Waziri Mkuchika ametangaza uamuzi huo kwenye kikao cha kamati kuu ya jimbo kilichokuwa na lengo la kuzungumzia mafanikio ya jimbo hilo.

Rais Samia ashiriki kwenye uapisho Namibia.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki hafla ya uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, iliyofanyika katika Ikulu ya Windhoek leo Machi 21, 2025. Nandi-Ndaitwah anakuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais wa Namibia tangu taifa hilo lipate uhuru wake tarehe 21 Machi 1990.

Sasa Unaweza kutusikiliza Online

Image
Kupitia platform/radio directories mbalimbali unaweza kusikiliza Radio Ngamia. pia kutufuata kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii @radiongamia

CAF yafungia uwanja wa Benjamin Mkapa

Image
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefungia kwa muda dimba la Benjamin Mkapa lililopo Dar es Salaam kutokana na eneo la kuchezea (pitch) kuendelea kupungua ubora wake. CAF imeelekeza maboresho ya uwanja huo yafayike haraka kufikia viwango vinavyotakiwa ili kuepuka Uwanja huo kufungiwa kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kati ya Simba SC dhidi ya Al Masry, imepangwa kuchezwa kwenye uwanja huo Aprili 9, 2024, hivyo basi CAF imelielekeza Shirikisho hilo kutuma jina la uwanja mbadala utakaotumiwa na vijana hao wa Msimbazi kufikia Machi 14, 2025. CAF imepanga kufanya ukaguzi katika uwanja huo wa Benjamin Mkapa, Machi 20, 2025 ili kuona maboresho yaliyofanyika kabla ya kufanya maamuzi ya matumizi yake.

AL AHLY WAMEWEKA MGOMO

Image
   Klabu ya Al Ahly imeomba kuahirisha mechi yake dhidi ya mpinzani wake Zamalek katika Ligi Kuu ya Misri iliyopangwa kufanyika leo saa 4:30 Usiku. Al Ahly katika taarifa yao waliyoichapisha mapema hii leo wametishia kujitoa kwenye Ligi ya Misri iwapo mechi yao dhidi ya Zamalek itachezeshwa na mwamuzi wa Misri ambapo anaamini waamuzi wa taifa hilo haasimamii haki na usawa katika ligi hiyo.  Al Ahly wamesema hawatacheza mechi hiyo hadi Chama cha soka nchini humo watakapoleta waamuzi kutoka nje ya mipaka ya Misri, na kusisitiza kwamba haitacheza ligi hiyo  endapo matakwa yake ya kutaka waamuzi kutoka nje ya nchi hayatatekelezwa. Al Ahly inashika nafasi ya 2 katika msimamo wa ligi kuu nchini Misri wakiwa na alama 39 tofauti ya alama 7 na Zamalek anayeshika nafasi ya 3. Ubaya Ubwela umefika kwenye dabi ya Cairo!

12 WAKAMATWA KWA JARIBIO LA KUVAMIA IKULU KENYA

Image
 Maafisa wa Polisi wa Kikosi maalum cha kumlinda Rais nchini Kenya Recce, wamewakamata vijana 12, waliokuwa wakijaribu kuingia katika Ikulu ya Nairobi. Kikosi cha maafisa hao kwa haraka kilizuia jaribio hilo la kuingia katika Ikulu ya Rais, ambalo ni eneo lenye ulinzi mkali, Mashahidi wanasema walishuhudia mvutano mkali kabla ya washukiwa hao kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.  Mamlaka bado haijafichua utambulisho au nia za watu waliohusika, lakini uchunguzi wa awali unaendelea. Vyombo vya usalama vimewahakikishia umma kwamba hakukuwa na tishio la haraka na usalama umeimarishwa zaidi katika Ikulu ya Rais na maeneo yaliyokaribu. Hata hivyo, haijabainika iwapo Rais Ruto alikuwa ndani ya Ikulu wakati wa tukio hilo la likitokea.