Mtandao warejea Tanzania

 


Hatimaye mtandao umerejea nchini Tanzania baada ya kufinywa kwa siku sita.


Hili imehjiri baada ya Rais Samia kuapishwa na kuchukua majukumu yake rasmi.

Katika hotuba aliyotoa wakati wa kuapishwa kwake Rais Samia alitoa maagizo kwa vyombo vya usalama kuhakikisha hali imerejea kama kawaida kwa Watanzania.

"Kamati ya kitaifa na kamata za ulinzi za mikoa na wilaya nawataka muhakikishe, kuanzia leo maisha ya wananchi yanarejea mara moja," alisema Rais Samia.

Kuzimwa kwa mtandao kuliathiri mawasiliano, biashara, kudorora kwa utalii mbali na hata kuwa vigumu kujua hali inavyoendelea nchini humo Tanzania.

Habari Zilizotrendi:

Zungu Spika Mpya wa Bunge la Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali mpya

MWIGULU NCHEMBA NDIYE WAZIRI MKUU MTEULE