Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali mpya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika siku yake ya kwanza ya kuanza rasmi muhula wake wa pili wa uongozi baada ya kula kiapo cha kuiongoza Tanzania, amemteua Bw. Hamza Said Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kupitia mitandao ya kijamii na Msemaji wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, imeelezwa kuwa Bw. Hamza Said Johari ataapishwa siku ya Jumatano, tarehe 5 Novemba 2025, saa 4:00 asubuhi, katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino, Dodoma.