Serikali ya Tanzania yatangaza kurejea kwa shughuli kama kawaida
Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa ametoa ujumbe kuwajulisha wananchi kuwa shughuli za kijamii na kiuchumi zinarejea kama kawaida kuanzia kesho, Jumanne tarehe 4 Novemba 2025.
"Wananchi wanaaswa kuendelea kuzingatia tahadhari ya miongozo ya kiusalama kadri itakavyokuwa inatolewa na vyombo vya Ulinzi na Usalama katika maeneo yao,"ujumbe huo umesema.
Katika hotuba ya kuapishwa kwake, Rais Samia aliagiza kurejea kwa hali ya kawaida mara moja.
