Posts

MWIGULU NCHEMBA NDIYE WAZIRI MKUU MTEULE

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu amempendekeza aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kinachosubiriwa kwa sasa baada ya jina kuwasilishwa kwa Spika wa Bunge ni mchakato wa kuthibitishwa kwa jina hilo na bunge

Zungu Spika Mpya wa Bunge la Tanzania

Image
  Mussa Azzan Zungu amechaguliwa kuwa Spika mpya wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zungu alipata kura 378 kati ya kura 383 zilizopigwa na wabunge katika mkutano wa kwanza na kikao cha kwanza cha bunge la 13 la Tanzania. Kwa ushindi huo, Mussa Azzan Zungu anakuwa Spika wa nane wa Bunge hilo tangu kuanzishwa kwake, baada ya kuwashinda wagombea wa vyama vingine waliopata jumla ya kura mbili pekee. Zungu aliteuliwa na chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwania nafasi hiyo, huku Spika, Dk. Tulia Ackson akijitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa sababu ambazo hazikuelezwa wazi. Zungu, atasaidiwa na Daniel Sillo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Spika. Miongoni mwa waliowahi kushika wadhifa huo wa Spika katika historia ya Tanzania ni Adam Sapi Mkwawa, Erasto Andrew Mbwana Mang’enya, Pius Msekwa, Samuel John Sitta, Anna Makinda, Job Ndugai, na Dk. Tulia Ackson.

Watu 12 wameuawa katika mlipuko wa kujitoa muhanga nje ya mahakama Pakistan

Image
  \ Takriban watu 12 wamefariki katika mlipuko uliotokea nje ya mahakama katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Mohsin Naqvi ameviambia vyombo vya habari kuwa watu 12 wamefariki na watu 27 wamejeruhiwa katika tukio hili. Mohsin Naqvi amesema, "Shambulio la kujitoa mhanga lilitokea mahakamani saa za jioni. Shambulio hili limesababisha uharibifu mkubwa, na watu 12 wameuawa na karibu 27 kujeruhiwa." Shirika la habari la Reuters lkimnukuu msemaji wa polisi akisema kuwa hali za baadhi ya waliojeruhiwa ni mbaya. Mlipuko huo ulitokea karibu na lango la Mahakama ya Wilaya ya Islamabad, ambayo kwa kawaida huwa na watu wengi wanaokuja mahakamani. Baada ya tukio hili, Waziri wa Ulinzi wa Pakistan Khawaja Asif amechapisha kwenye Instagram akisema kuwa Pakistan iko katika hali ya vita. Aliandika kwenye X, "Ikiwa mtu yeyote anafikiri kwamba Jeshi la Pakistan linapigana vita katika eneo la mpaka wa Afghanistan na Pakistani na maeneo ya mbali ya Balo...

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali mpya

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika siku yake ya kwanza ya kuanza rasmi muhula wake wa pili wa uongozi baada ya kula kiapo cha kuiongoza Tanzania, amemteua Bw. Hamza Said Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kupitia mitandao ya kijamii na Msemaji wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, imeelezwa kuwa Bw. Hamza Said Johari ataapishwa siku ya Jumatano, tarehe 5 Novemba 2025, saa 4:00 asubuhi, katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Kanali Mamadi Doumbouya atangaza kugombea urais Guinea licha ya ahadi ya kutowania

Image
Kanali Mamadi Doumbouya aliyenyakua madaraka Guinea kupitia mapinduzi ya kijeshi miaka minne iliyopita,atashiriki katika uchaguzi wa rais licha ya kuahidi hapo awali kuwa hatawania urais na atarejesha utawala wa kiraia. Kanali Doumbouya aliwasili katika mahakama ya juu hapo jana Jumatatu akiwa amendamana na wanajeshi kuwasilisha rasmi azma yake ya kugombea urais. Vyama viwili vikuu vya upinzani vimepigwa marufuku kushiriki katika uchaguzi huo unaotarajiwa mwezi ujao Desemba. Waguinea walishangazwa na tangazo kuwa wagombea urais watahitajika kulipa ada ya dola laki moja kushiriki katika uchaguzi huo. Mnamo Septemba mwaka 2021,mapinduzi ya kushtukiza ya kijeshi yalifanyika nchini Guinea nakumaliza hatamu yenye utata ya Rais Alpha Conde, chini ya mwaka mmoja baada ya kushinda muhula wa tatu uliogubikwa na maandamano mabaya na ukandamizaji mkali dhidi ya upinzani katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.

Mtandao warejea Tanzania

Image
  Hatimaye mtandao umerejea nchini Tanzania baada ya kufinywa kwa siku sita. Hili imehjiri baada ya Rais Samia kuapishwa na kuchukua majukumu yake rasmi. Katika hotuba aliyotoa wakati wa kuapishwa kwake Rais Samia alitoa maagizo kwa vyombo vya usalama kuhakikisha hali imerejea kama kawaida kwa Watanzania. "Kamati ya kitaifa na kamata za ulinzi za mikoa na wilaya nawataka muhakikishe, kuanzia leo maisha ya wananchi yanarejea mara moja," alisema Rais Samia. Kuzimwa kwa mtandao kuliathiri mawasiliano, biashara, kudorora kwa utalii mbali na hata kuwa vigumu kujua hali inavyoendelea nchini humo Tanzania.

Serikali ya Tanzania yatangaza kurejea kwa shughuli kama kawaida

Image
  Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa ametoa ujumbe kuwajulisha wananchi kuwa shughuli za kijamii na kiuchumi zinarejea kama kawaida kuanzia kesho, Jumanne tarehe 4 Novemba 2025. "Wananchi wanaaswa kuendelea kuzingatia tahadhari ya miongozo ya kiusalama kadri itakavyokuwa inatolewa na vyombo vya Ulinzi na Usalama katika maeneo yao,"ujumbe huo umesema. Katika hotuba ya kuapishwa kwake, Rais Samia aliagiza kurejea kwa hali ya kawaida mara moja.

Mamlaka Sudan yashughulikia athari za maporomoko ya ardhi

Image
  Timu za uokoaji kwa kushirikiana na wakaazi wa eneo la milima ya Jebel Marra jimbo la Darfur zinaendelea na juhudi za kuopoa miili, ingawa wanakumbwa na changamoto kubwa kutokana na ukosefu wa vifaa na ukubwa wa janga hilo. Kulingana na takwimu rasmi idadi ya watu waliopoteza maisha katika mkasa huo inakadiriwa kuwa kati ya watu 300 na 1,000. Baraza la mpito la uongozi wa kijeshi chini ya usimamizi wa Jenerali Abdel Fattah al-Burhan limeahidi kuhamisha raslimali zote zilizopo ili kusaidia waathiriwa, wakati serikali pinzani ikitangaza iko tayari kuanza juhudi za kutoa misaada.

Wagonjwa wa Uviko-19 Waongezeka

Image
  Wizara ya Afya imetoa taarifa yake ambapo imeonyesha ongezeko la watu wenye maambukizi ya ugonjwa wa Uviko-19 nchini katika kipindi cha mwezi Februari hadi Aprili mwaka huu. Takwimu hizo zimetolewa leo Jumanne Mei 20, 2025, na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Grace Magembe kupitia taarifa yake kwa umma, ambapo amesema kumekuwepo ongezeko la tetesi zinazohusiana na magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa katika jamii nchini. “Hali ya kuongezeka na kupungua kwa ugonjwa huu imekuwepo kila mwaka tangu kutangazwa kwa ugonjwa huu mwaka 2020. Kwa kipindi hiki ongezeko hili linaonekana zaidi katika Mkoa wa Dar es Salaam,” amesema Dk. Magembe. Dk. Magembe amesema kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya mfumo njia ya hewa, wizara imebaini kuna ongezeko la wagonjwa wenye Uviko-19 kutoka wawili kati ya watu 139 waliopimwa Februari sawa na asilimia 1.4 hadi wagonjwa 31 kati ya watu 185 waliopimwa Aprili mwaka huu, sawa na asilimia 16.8. “Tangu Februari hadi Aprili 2025, ufuatiliaji wa viru...

Waziri Mkuu afanya ukaguzi wa viwanja

Image
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefanya ukaguzi wa viwanja vitakavyotumiwa kufanya mazoezi na timu zitakazoshiriki michuano ya CHAN ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Agosti mwaka huu pamoja na michuano ya AFCON 2027 ikiwa ni ushirikiano wa nchi tatu, Tanzania, Kenya na Uganda. Baada ya ukaguzi huo Waziri Mkuu, amewaagiza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufanya tathmini ya kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya mazoezi vitakavyotumika kwenye michuano hiyo. Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo jana Machi 29, 2025 baada ya kupokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata ambao ndiyo wakandarasi wa mradi huo.

Maafisa na Askari JWTZ Wavishwa nishani

Image
  Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Jacob Mkunda, kwa niaba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan, amewavisha nishani mbalimbali maafisa na askari wa JWTZ jijini Mbeya leo, Machi 26, 2025. Akizungumza baada ya kuvisha nishani hizo, Jenerali Mkunda amewapongeza maafisa na askari waliotunukiwa kwa jinsi Rais Samia Suluhu Hassan alivyotambua mchango wao katika kulitumikia taifa kwenye nyanja ya ulinzi. Aidha, amewataka maafisa na askari kuendelea kuviishi viapo vyao na kuhakikisha mipaka yote ya nchi inabaki salama wakati wote. Nishani walizotunukiwa askari hao ni Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne, Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ, na Nishani ya Jumuiya ya SADC

Ujumbe wa Rais Samia kwa Rais wa Zambia

Image
  Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama siku ya jana March 24, 2025 amewasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Haikainde Hichielema katika Ikulu ya Rais iliyopo Jijini Lusaka Zambia. Rais Hichielema amemshukuru Rais Samia kwa ujumbe huo maalum na kubainisha ya kuwa Zambia na Tanzania ni nchi zenye historia na ushirikiano wa kindugu muda mrefu na usio na mipaka. Waziri Mhagama akiwa ameambatana na ujumbe wake akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Generali Mathew Edward Mkingule amemshukuru Rais Hichielema kwa mapokezi mazuri na ushirikiano imara ulipo baina ya Tanzania na Zambia

CEO WA SAMSANG AFARIKI

Image
  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya teknolojia ya Korea Kusini, Samsung Electronics, Han Jong-Hee, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63. Kulingana na msemaji wa kampuni hiyo aliyezungumza na kituo cha habari cha CNN, Han amefariki dunia baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo (cardiac arrest) uliomsababishia umauti leo Jumanne Machi 25, 2025. Han Jong-Hee alizaliwa mwaka 1962 na alijiunga na kampuni ya Samsung Electronics mwaka 1988 baada ya kumaliza Shahada yake ya Kwanza ya Uhandisi wa Umeme katika Chuo Kikuu cha Inha nchini Korea Kusini. Tangu mwaka 2022, aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, akisimamia maeneo ya vifaa vya kielektroniki vya nyumbani na simu za mkononi.

Vipimo 5,600 vyakutwa na Dosari

Image
  Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) umefanya uhakiki wa vipimo milioni 3.6 katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye mita za maji, vituo vya kuuzia mafuta na mitungi ya gesi, katika kipindi cha miaka minne ambapo katika uhakiki huo vipimo 100,005 vilikutwa na mapungufu na kurekebishwa na vipimo vingine 5,600 vilikutwa na dosari. Mtendaji Mkuu wa WMA, Albani Kiula amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wakala huo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita. Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Wakala wa Vipimo litakalorahisisha, kuboresha na kusogeza huduma karibu na wananchi.

Tanzania yaanza safari kuitambulisha Singeli kimataifa

Image
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali imedhamiria na imeanza safari ya kuupeleka muziki wa Singeli kimataifa, ili uorodheshwe katika utamaduni usioshikika kwenye Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Msigwa amesema hayo mkoani Dar es Salaam, wakati akifungua rasmi warsha ya Uteuzi wa Urithi wa Utamaduni Usioshikika iliyoendeshwa na UNESCO na kushirikisha wadau mbalimbali wa muziki, viongozi wa Serikali na wataalamu wa utamaduni. Msigwa amesema muziki wa Singeli una uwezo mkubwa wa kuchochea maendeleo na kuleta umoja katika jamii ikiwa utazingatia maadili na kuakisi utambulisho wa Taifa la Tanzania. Aidha, amelitaka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) chini ya Katibu Mtendaji wake Dkt. Kedmon Mapana kuhakikisha linasimamia kikamilifu maadili katika muziki wa Singeli ili kuufanya uwe na hadhi inayostahili duniani.

DARAJA LA MAGUFULI KUANZA KAZI MWEZI APRIL

Image
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt. Charles Msonde amesema daraja la J.P Magufuli (Kigongo Busisi) lenye urefu wa KM 3 litaanza kutumika rasmi Aprili 30 mwaka huu. Hata hivyo, amesema ifikapo Aprili 10, 2025 magari yataanza kupita upande mmoja kwenye daraja hilo ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 97 huku ujenzi wake ukigharimu zaidi Shilingi ya bilioni 610. Daraja hilo limejengwa kwa lengo la kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara - Sengerema Geita KM90 ambayo ni sehemu ya barabara iliyopo kwenye Ushoroba wa Ziwa Victoria inayoanzia Sirari mpakani mwa Tanzania na Kenya hadi Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda. Kwa sasa sehemu ya barabara hiyo eneo la Kigongo Busisi inaunganishwa kwa kutumia vivuko vikubwa vitatu vya MV Mwanza, MV Misungwi na MV Sengerema. Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 3 na upana wa meta 28.45 lina njia mbili za magari zenye upana wa mita 7 kila upande.

Mkuchika atangaza kutogombea Ubunge

Image
  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalumu George Mkuchika ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini mkoani Mtwara ametangaza rasmi kutogombea ubunge katika uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu. Waziri Mkuchika ametangaza uamuzi huo kwenye kikao cha kamati kuu ya jimbo kilichokuwa na lengo la kuzungumzia mafanikio ya jimbo hilo.

Rais Samia ashiriki kwenye uapisho Namibia.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki hafla ya uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, iliyofanyika katika Ikulu ya Windhoek leo Machi 21, 2025. Nandi-Ndaitwah anakuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais wa Namibia tangu taifa hilo lipate uhuru wake tarehe 21 Machi 1990.

Sasa Unaweza kutusikiliza Online

Image
Kupitia platform/radio directories mbalimbali unaweza kusikiliza Radio Ngamia. pia kutufuata kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii @radiongamia

CAF yafungia uwanja wa Benjamin Mkapa

Image
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefungia kwa muda dimba la Benjamin Mkapa lililopo Dar es Salaam kutokana na eneo la kuchezea (pitch) kuendelea kupungua ubora wake. CAF imeelekeza maboresho ya uwanja huo yafayike haraka kufikia viwango vinavyotakiwa ili kuepuka Uwanja huo kufungiwa kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kati ya Simba SC dhidi ya Al Masry, imepangwa kuchezwa kwenye uwanja huo Aprili 9, 2024, hivyo basi CAF imelielekeza Shirikisho hilo kutuma jina la uwanja mbadala utakaotumiwa na vijana hao wa Msimbazi kufikia Machi 14, 2025. CAF imepanga kufanya ukaguzi katika uwanja huo wa Benjamin Mkapa, Machi 20, 2025 ili kuona maboresho yaliyofanyika kabla ya kufanya maamuzi ya matumizi yake.